Jeremiah 31:8-9

8 aTazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini
na kuwakusanya kutoka miisho ya dunia.
Miongoni mwao watakuwepo vipofu na viwete,
mama wajawazito na wenye utungu wa kuzaa.
Umati mkubwa wa watu utarudi.
9 bWatakuja wakilia;
wataomba wakati ninawarudisha.
Nitawaongoza kando ya vijito vya maji
katika mapito yaliyo tambarare ambapo hawatajikwaa,
kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli,
naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.
Copyright information for SwhNEN